FM Manyara

Manyara, Tanga, Kilimanjaro katika oparesheni barabarani

20 October 2026, 4:34 pm

Picha ya baadhi ya viongozi wa usalama Barabarani

Madereva kanda ya kaskazini wametakiwa kufuata sheria na taratibu za usalama barabarani, ikiwa ni pamoja na kuimarisha uwajibikaji kwa lengo la kupunguza na kutokomeza ajali za barabarani .

Na Emmy Peter

Makamanda wa usalama barabarani kutoka mikoa ya Manyara, Tanga na Kilimanjaro wamefanya operesheni maalumu ya kukagua mabasi ya safari za usiku yanayoelekea mikoani kwa lengo la kudhibiti makosa ya usalama barabarani na kupunguza ajali .

Aikizungumzia oparesheni hiyo Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Manyara, Mrakibu wa polisi Michael Mwakasungula, Amesema hatua hiyo ni sehemu ya kuhamasisha madereva kuendelea kufuata sheria na taratibu za usalama barabarani, ikiwa ni pamoja na kuimarisha uwajibikaji kwa lengo la kupunguza na hatimaye kutokomeza ajali za barabarani nakusema wameendelea kutoa zawadi kwa baadhi ya madereva wanaozingatia sheria za usalama barabarani kwa hiari bila kulazimishwa.

Sauti ya Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Manyara, Mrakibu wa polisi Michael Mwakasungula,

Kwa upande wake kamanda wa polisi kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro ACP Nassoro Sisiwaya amesema hatua hiyo inalenga kudhibiti ajali za barabarani hasa kuelekea kipindi cha mwisho wa mwaka ambapo amewataka madereva kuzingatia sheria na taratibu za usalama barabarani ili kulinda maisha ya abiria na watumiaji wengine wa barabara.

Sauti ya kamanda wa polisi kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro ACP Nassoro Sisiwaya

Aidha Mkuu wa Kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Tanga Mrakibu wa polisi mwandamizi Willy Mwamasika, amesema wameendelea kuchukua hatua dhidi ya makosa mbalimbali ya usalama barabarani, ikiwemo mwendo kasi, kubeba abiria kupita kias i pamoja na kuyapita magari bila kufuata utaratibu.

Sauti ya mkuu wa Kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Tanga Mrakibu wa polisi mwandamizi Willy Mwamasika,