FM Manyara

Manyara yaadhimisha Muungano kwa kuliombea Taifa

April 25, 2024, 10:29 pm

Picha ya viongozi wa mkoa wa Manyara na wilaya ya Babati.

Maadhimisho ya Muungano yafanyika mkoani Manyara kwa dua maalumu na kukemea vitendo vya ukatili vinavyoendelea kushamiri kwa watoto na kinamama.

Na George Agustino

Mkoa wa Manyara leo umeadhimisha maadhimisho ya miaka 60 ya  muungano wa Tanganyika na zanzibar kwa kufanya dua maalumu ya kuliombea taifa pamoja na viongozi wa nchi ili inchi izidi kuwa na amani pamoja na  utulivu  .

Maadhimisho hayo yamefanyika leo katika uwanja wa Tanzanite kwaraa uliopo mjini Babati mkoani hapa na kuongozwa na katibu Tawala mkoa wa Manyara Mariam Muhaji na nakuhudhuria ni viongozi mbalimbali wa serikali, viongozi wa dini na wananchi 

Katika maadhimisho hayo amekemea vitendo vya ukatili wa kijinsia na watoto unaoendelea katika mkoa wa manyara na kuwataka wananchi kila mmoja kukemiea vitendo hivyo katika jamii wanazoishi.

Sauti ya katibu Tawala mkoa wa Manyara

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Babati  Lazaro Jacobo Twange amewashukuru viongozi wa dini kwa kuwa bega kwa bega  kwa kuwaombea na kuliombea Taifa ambapo  amewataka wananchi kuwa wavumilivu wakati huu ambao serikali inajitahidi kurekebisha miundombinu ya barabara iliyoharibiwa na mvua za masika zinazoendelea kunyesha nchini,

Sauti mkuu wa wilaya ya Babati