FM Manyara

Mitandao ya kijamii yachangia mmomonyoko wa maadili

April 18, 2024, 11:44 am

Meneja wa TCRA kanda ya kaskazini Mhandisi Fransis Mihayo akiwa studio za FM Manyara. Picha na George Augustino

Sababu ya kuongezeka kwa mmomonyoko wa maadili kwa watoto yatajwa wazazi ndio sababu kubwa kwa kuwaachia simu za mkononi watoto wao.

Na George Augustino

Jamii mkoani Manyara imetakiwa kuwalea watoto wao katika misingi imara na yenye maadili  ya kitanzania kwa kuwaepusha kutumia  simu za mkononi  ili kujenga kizazi chenye maadili mema  na kuepuka  kesi za mitandao ya kijamii.

Hayo yamesemwa  leo na Meneja wa Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA kanda ya kaskazini Mhandisi Fancisi  Mihayo alipokuwa akiongea katika kipindi cha Mseto wa leo kinachorushwa na Fm Manyara Radio, amesema  asilimia kubwa kwa  sasa  watoto wanalelewa na simu  za mkononi ambapo wazazi huwapa watoto wao uhuru wakutumia simu nakuingia katika kurasa za  mitandao ya kijamii hali ambayo si nzuri kwa malezi ya mtoto.

Sauti ya Fransis Mihayo

Aidha, Injia Mihayo amewataka wazazi kuwa makini katika malezi ya watoto wao kwa kudhibiti matumizi ya simu na kuacha kuweka picha ambazo hazina maadili katika mitandao yao ya kijamii.

Sauti ya Fransis Mihayo