FM Manyara

Takukuru Manyara yaokoa zaidi ya shilingi 44m

April 24, 2024, 12:29 pm

Picha ya Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru mkoa wa Manyara Suzana Raymond 

Katika kipindi cha  kuanzia mwezi March hadi April 2024  kiasi cha shilling Millioni arobaini na nne zimeokolewa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru kutoka wilaya ya kiteto, mbulu na ofisi ya mkoa

Na George Agustino

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru mkoa wa Manyara imeokoa zaidi ya shilingi Millioni arobaini na nne kwa kipindi cha kuanzia mwezi januari hadi machi mwaka 2024 kupitia ofisi ya takukuru wilaya ya kiteto, mbulu na ofisi ya mkoa wa Manyara

Taarifa hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru mkoa wa Manyara Suzana Raymond alipokuwa  akizungumza  na waandishi wa habari ofisini kwake, amesema, kati ya fedha hizo kiasi cha zaidi ya shilingi  Millioni ishirini na tisa zilikuwa ni fedha zilizokusanywa katika Halmashauri ya wilaya ya kiteto kupitia mashine za pos.

Sauti ya Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru mkoa wa Manyara 

Aidha Suzana amesema katika Halmashauri ya wilaya ya mbulu kiasi cha shillingi milioni nane sitini na nne elfu na mia nne sabini na nne ambazo ni kodi ya zuio ziliwasilishwa Mamlaka ya mapato Tanzania TRA baada ya ufuatiliaji.