FM Manyara

CCM yashindwa kusimamia miundombinu ya stendi ya Noah Babati mji

May 3, 2024, 6:45 am

Picha ya ya stand ya noah mjini Babati

Licha ya juhudi za wafanyabiashara mbali mbali wakiwemo mama lishe wanaofanya biashara zao katika stendi ya Noah iliyopo Babati mji kuomba uwongozi wa Chama cha Mapinduzi Ccm Babati mji kuboresha  mazingira  ya eneo hilo linalotuama maji machafu nakuhatarisha afya zao lakini juhudi zao zimegonga mwamba.

Na Marino Kawishe

Wananchi wanaofanya biashara katika eneo la stend ya Noah lililopo katika kata ya Bagara  Halmashauri ya mji  wa Babati wameiomba serikal ya Chama cha Mapinduzi Ccm kuboresha miuondo mbinu ya eneo hilo linalotuama maji machafu yanayotishia  afya zao pamoja na kuomba kujengewa choo kwenye eneo hilo

Picha ya eneo la stend ya Noah lililopo katika kata ya Bagara  Halmashauri ya mji wa Babati

Wakizungumza na Fm Manyara wafanyabiashara hao wamesema wanafanya biashara zao kwa tabu katika eneo hilo kutokana na maji kutuama hali inayopelekea kutoa harufu kali inayoambatana na mazingira machafu licha yalikupa kodi pamoja na ushuru kwa wasimamizi wa eneo hilo lakini mpaka sasa hakuna  juhudi zozote  zilizo chukuliwa katika eneo hilo,. 

Sauti ya Wafanyabiashara

Kwa upende wake katibu wa Chama cha Mapinduzi Ccm Babati mji Mohamed Chollaje alipotafutwa na mwandishi wa habari hii ili kuzungumzia swala hilo alishindwa kutoa ushirikiano na badala yake alisema yupo kwenye kikao licha kutafutwa kwa mara nyingine.

Sauti ya katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Babati

Aidha, Afisa afya wa Halmashauri ya Mji wa Babati Emmanuel Kimonge amesema  eneo hilo lipo chini ya Chama cha Mapinduzi Ccm ambapo wameshawaandikia barua kwaajili ya kuweka vifusi  katika eneo hilo ili kuweka mazingira salama na wamewaelekeza mama lishe kufuata taratibu za kiafya kwa kuwa na vyakula vya moto pamoja na maji ya moto ili kuwa salama.

Sauti ya Afisa afya wa Halmashauri ya Mji wa Babati