FM Manyara

Polisi na Wananchi Manyara waimarisha ushirikiano

10 May 2026, 12:40 pm

Picha ya baadhi ya familia za polisi pamoja na viongozi mbalimbali

Wananchi mkoani Manyara wameungana na askari wa jeshi la polisi pamoja na familia zao katika kusherehekea siku ya familia ya polisi kwa lengo la kujenga mshikamano na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa askari wa jeshi la polisi.

Na Mzidalfa Zaid

Hafla hiyo ambayo imefanyika jana may 09 ,2026  katika viwanja vya FFU mkoa wa Manyara imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wananchi,familia za askari wa jeshi la polisi ambapo  Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Manyara Lucas Mwakatundu, amesema siku hiyo ni maalum kutokana na wananchi wanavyotoa ushirikiano kwa jeshi la polisi na kupelekea nchi kuwa na amani.

sauti ya Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Manyara Lucas Mwakatundu
picha ya Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Manyara Lucas Mwakatundu

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni mbunge wa jimbo la Babati mjini Emmanuel Khambay , amelipongeza jeshi la polisi kwa kuendelea kupambana na uhalifu na kuhakikisha usalama unakuwepo na kuahidi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo.

sauti ya mbunge wa jimbo la Babati mjini Emmanuel Khambay
picha ya mbunge wa jimbo la Babati mjini Emmanuel Khambay

Aidha, katika hafla hiyo kumefanyika michezo mbalimbali ambapo washindi wa michezo hiyo wamejinyakulia zawadi mbalimbali huku baadhi ya maaskari wa jeshi la polisi wakitunukiwa zawadi za utendaji bora wa kazi ambapo baadhi yao wamepongeza hatu hiyo kwani inatoa motisha ya kuongeza juhudi za  utendaji kazi.

sauti ya baadhi ya maaskari waliopata zawadi