FM Manyara
FM Manyara
1 May 2026, 7:39 pm

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga, ameipongeza Kampuni ya MATI Super Brand ya mjini Babati mkoani Manyara kwa kuwaajiri vijana wengi na kupunguza changamoto ya vijana kuwa tegemezi .
Na Mzidalfa Zaid
Sendiga amesema hayo leo katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani ambayo yamefanyika katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa, amesema amefuarahishwa na uwekezaji huo na kuwataka wawekezaji wengine kuiga mfano huo.
Kwa upade wake Mkurugenzi wa kampuni ya MATI David Mulokozi amesema kampuni ya mati wameadhimishwa siku hii kwa kishindo huku akielezea dhamira yake ya kukuza uchumi wa Tanzania kupitia sekta ya viwanda, utalii na hifadhi za mazingira.
Aidha, katika maonyesho hayo, Kampuni ya MATI Super Brand imejinyakulia kombe pamoja na zawadi mbalimbali ikiwemo banda bora na maandamano bora.
