FM Manyara
FM Manyara
21 July 2026, 4:41 pm

Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kushiriki Maonesho ya 32 ya Nane Nane Kanda ya Kaskazini yanayotarajiwa kufanyika katika Viwanja vya Njiro, mkoani Arusha, ili kujionea teknolojia mbalimbali za kilimo na mifugo pamoja na fursa zinazopatikana katika sekta hizo.
Na Mzidalfa Zaid
Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake. Amesema wakulima, wafugaji na wadau wengine wanaotaka kushiriki maonesho hayo wanapaswa kujisajili mapema ili kukamilisha taratibu za ushiriki.
Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara anayeshughulikia Idara ya Huduma za Uchumi na Uzalishaji, Faraja Ngerageza, amesema kaulimbiu ya Maonesho ya Nane Nane mwaka 2026 ni: “Tambua Soko, Ongeza Tija, Tekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.”
