FM Manyara
FM Manyara
26 May 2026, 6:21 pm

Waumini wa dini ya Kiislamu mkoani Manyara wametakiwa kushiriki swala ya Eid itakayofanyika kimkoa katika viwanja vya Tanzanite Kwaraa stadium huku wakihimizwa kujitokeza kwa wingi na kuendelea kutenda matendo mema katika siku hiyo ya eid.
Na Mzidalfa Zaid
Hayo yamesemwa na Sheikh wa Mkoa wa Manyara, Mohamed Kadidi wakati akizungumza kuhusu maandalizi ya swala la Eid linalotarajiwa kufanyika kesho ambapo amewataka waumini wa dini ya kiislamu kufika maeneo hayo kuanzia saa moja asubuhi.
Aidha, Sheikh Kadidi amewataka wananchi kutumia siku ya Eid kufanya matendo mema ikiwemo kusaidiana, kuoneshana upendo pamoja na kudumisha amani na mshikamano katika jamii.