FM Manyara

Wananchi Manyara wahimizwa kuweka akiba ya chakula

23 July 2026, 4:35 pm

Picha ya Kaimu Katibu Tawala wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Manyara, Faraja Ngerageza, 

Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kuweka akiba ya mazao ya chakula ili kujikinga na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya tabianchi yanayoathiri uzalishaji wa mazao katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Na Mzidalfa Zai

Wito huo umetolewa leo na Kaimu Katibu Tawala wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Manyara, Faraja Ngerageza, ambaye amesema kuwa utunzaji wa akiba ya mazao ya chakula utasaidia kuhakikisha kaya zinaendelea kuwa na chakula cha kutosha hata pale uzalishaji utakapopungua kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Sauti ya Kaimu Katibu Tawala wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Manyara, Faraja Ngerageza

Aidha, Ngerageza amewataka wafanyabiashara kuzingatia sheria na kanuni za ulipaji wa ushuru, akisisitiza kuwa kulipa ushuru kwa wakati ni wajibu wa kila mfanyabiashara na kunachangia kuongeza mapato ya serikali kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma za maendeleo kwa wananchi.