FM Manyara
FM Manyara
17 September 2026, 9:43 pm

Mwamposa awaombea viongozi na wananchi wa manyara, atoa wito wa ushirikiano.
Na Mzidalfa Zaid
Mtume Bonifasi Mwamposa amefika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara na kutoa baraka kwa Mkuu wa Mkoa Martin Shigela, pamoja na watumishi wa ofisi hiyo.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mtume Mwamposa amewaombea viongozi na watumishi wa Mkoa wa Manyara, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana katika kuwahudumia wananchi na kutekeleza majukumu ya maendeleo.
Aidha, Mtume Mwamposa ameuomba Mkoa wa Manyara kutenga maeneo makubwa ya wazi yatakayoweza kutumika kwa shughuli mbalimbali za serikali na shughuli za kijamii, hatua ambayo amesema itasaidia kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Martin Shigela, amemshukuru Mtume Mwamposa kwa kufika ofisini hapo na kuwaombea viongozi pamoja na watumishi wa Mkoa, akieleza kuwa baraka na maombi ni sehemu muhimu katika kuwatia moyo watumishi katika kutekeleza majukumu yao.