FM Manyara
FM Manyara
7 September 2026, 7:32 pm

Shirika la umeme Tanzania TANESCO mkoa wa Manyara kwa kushirikiana na jeshi la polisi limewakamata watu watatu wa kitongoji Cha Ndoroboni kijiji cha Kiru six kwa tuhuma za kuunganishiwa umeme kinyume na Sheria .
Na Mzidalfa Zaid
Afisa uhusiano TANESCO mkoa wa Manyara Samwel Mandar amesema TANESCO inaendelea na msako wa kukagua miundombinu ya shirika ikiwemo kukagua mita nakubaini kama kuna wananchi wamejiunganishia umeme kinyume cha sgeria, ambapo amesema watuhumiwa hao wameweka mita feki ambazo hazionyesh i matumizi ya umeme.
Msimamizi wa kitengo Cha udhibiti mapato TANESCO mkoa wa Manyara Maisha Mchuruza amesema watu hao wameunganishiwa umeme bila kufuata utaratibu wa Tanesco na kuwaonya wananchi kuacha tabia hiyo mara moja.
Baadhi ya watuhumiwa ambao wameunganishiwa umeme wamesema waliunganishiwa na mtu Mmoja ambae alijifanya mfanyakazi wa Tanesco na kuwaambia watoe pesa ili waunganishiwe umeme.

Mwenyekiti wa kitongoji cha ndoroboni kijiji cha Kiru six Ramadhani Juma amesema hana taarifa za wananchi hao kuunganshiwa umeme, ambapo amewataka wananchi wake kufuata hatua zote za kuunganishiwa umeme.
