FM Manyara
FM Manyara
20 September 2026, 12:33 pm

Serikali mkoani Manyara imeupongeza uongozi wa shule ya Greenland iliyopo wilayani Babati mkoani Manyara kwa kutoa elimu Bora .
Na Emmy Peter
Shule ya Green Land iliyopo Riroda mkoani Manyara, imefanya mahafali ya wanafunzi wa Darasa la Saba, ambapo Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Manyara, Mugisha Galibona, alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo ambapo ameupongeza uongozi wa shule hiyo kwa juhudi zake katika kutoa elimu na malezi kwa wanafunzi.
Akizungumza katika mahafali hayo yaliyofanyika shuleni hapo, Galibona ameahidi kushirikiana na uongozi wa shule hiyo katika juhudi za kuanzisha shule ya Sekondari, ili kuwawezesha wanafunzi wanaohitimu Darasa la Saba kuendelea kupata elimu na malezi katika mazingira bora.

Mkurugenzi wa Shule ya Green Land, Delifin, amesema uongozi wa shule hiyo una mpango wa kuanzisha shule ya Sekondari, hatua itakayowawezesha wanafunzi wanaomaliza Darasa la Saba kuendelea na masomo katika shule hiyo, huku wakiendelea kupata malezi na kuendeleza misingi ya elimu waliyojengewa.
Kwa upande wao wahitimu hao kupitia risala yao, wameushukuru uongozi wa Shule ya Green Land kwa kuwapatia elimu, malezi na usimamizi mzuri katika kipindi chote cha masomo yao.

