FM Manyara

Shirika la Hand in Hand lasaidia wafuga kuku Manyara

24 June 2026, 1:01 am

Picha ya Meneja wa Shirika la Hand in Hand tawi la Manyara Yona Onna akizungumza na washiriki wa jukwaa la kibiashara

Wafugaji na wanunuzi wa kuku Wilayani Babati mkoani Manyara wamelishukuru Shirika la Hand in Hand kwa kuwakutanisha pamoja kujadili juu ya mahusiano ufugaji na soko la kuku.

Na Christina Christian

Wakizungumza kwenye jukwaa la mahusiano ya kibiashara kwa wadau katika soko la kuku lililofanyika  wilayani Babati wamesema jukwaa hili linakwenda kuwafungulia fursa mbalimbali za kibiashara kwani wamekutana limewaunganisha pamoja kibiashara.

Wamesema Shirika la Hand in Hand limekuwa msaada mkubwa kwao kwani wanafuga kisasa na kuwarahisishia katika masoko na mnunuzi kupata kuku bora kutoka moja kwa moja kwa mfugaji

Sauti ya wadau

kwa upande wake Meneja wa Shirika la Hand in Hand tawi la Manyara Yona Onna amesema kuwa lengo la jukwaa hili ni kuwakutanisha pamoja ili kuweza kujenga na kufahamu changamoto wanazokutananazo ili kuzitafutia ufumbuzi

Sauti ya Meneja wa Shirika la Hand in Hand tawi la Manyara
Picha ya Viongozi wa Shirika la Hand in Hand pamoja na Wadau walioshishiriki jukwaa la mahusiano ya kibiashara