FM Manyara

Manyara yaadhimisha miaka 62 ya muungano kwa kufanya shughuli za kijamii

25 April 2026, 11:50 am

picha ya baadhi ya watumishi pamoja na wananchi wakishiriki zoezi la usafi

Mkoa wa Manyara umeaadhimisha miaka  62 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar  kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii  ikiwemo upandaji wa miti , kufanya usafi  katika halmashauri  ya mji wa babati pamoja na kufanya michezo mbalimbali.

Na Mzidalfa Zaid

Akiongea kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga,mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda, amewataka wananchi kuendelea kuimarisha amani na mshikamano.

Amesema Taifa la Tanzania limeendelea kuwa mfano wa utulivu wa kisiasa,mshikamano wa kijamii , na maendeleo ya kijamii ambapo yote hayo yamesababishwa na umoja uliwekwa na mwalimu julias nyerere na shekhe amani karume.

sauti ya mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda

Kwa upande wake katibu tawala mkoa wa Manyara Mariam Muhaj, amesema katika kuadhimisha siku hiyo wamepanda miti katika maeneo mbalimbali ya mkoa , kufanya usafi pamoja na mazoezi.

sauti ya katibu tawala mkoa wa Manyara Mariam Muhaj
picha ya katibu tawala mkoa wa Manyara Mariham Muhaj akifanya usafi

Nao baadhi ya wazee kutoka mkoani Manyara ambao walishuhudia  muungano huo mwaka 1964, wamesema wamefurahia uwepo wa muungano kutokana na umoja na amani iliyopo.

sauti ya baadhi ya wazee

Maadhimisho ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar huadhimishwa april 26 kila mwaka, na kwa mkoa wa Manyara maadhimisho hayo yameadhimishwa leo  na kauli mbiu ya miaka 62 ya muungano  kwa mwaka huu  ni amani, umoja na mshikamano ni msingi wa  maendeleo  endelevu.

picha ya baadhi ya wananchi wakifanya usafi
picha ya baadhi ya viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wakifanya usafi