FM Manyara

DED Babati TC akabidhi pikipiki kwa maafisa maendeleo

5 May 2026, 7:46 pm

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati CPA. Shaaban Mpendu akikabidhi piki piki

Wataalam wa Idara ya Maendeleo ya Jamii ngazi ya Kata Halmashauri ya Mji wa Babati wamekabidhiwa Pikipiki ili kuongeza ufanisi zaidi katika utendaji kazi.

Na Mzidalfa Zaid

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati CPA. Shaaban Mpendu amekabidhi Pikipiki 5 aina ya Boxer 150 HD zenye jumla ya Shilingi Milioni 19 kwa Maafisa Maendeleo wa Jamii ngazi ya Kata kwa lengo la kurahisisha utendaji wa kazi

Sauti ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati CPA. Shaaban Mpendu

Aidha Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Ally Mwinyikombo ameeleza kuwa mchakato wa manununuzi ya Pikipiki kwa Kata tatu zilizosalia unaendelea kufanyiwa kazi.