FM Manyara

Wananchi Manyara watakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya Ebola

19 May 2026, 4:56 pm

picha ya mratibu wa huduma za tiba mkoa wa Manyara Elford  Mukerebe na afisa afya mkoa wa manyara Suten Mwabulambo

Wananchi mkoani Manyara, wametakiwa kuchukua tahadhari ya ugonjwa Ebola unaosababishwa na virusi vya Ebola kutokana na ugonjwa huo kuwa miongoni mwa magonjwa ya milipuko, kufuatia  ugonjwa  huo kuwa  tishio  katika baadhi ya nchi za afrika mashariki ikiwemo nchi ya Uganda na Congo.

Na Mzidalfa Zaid

Wito huo umetolewa na mratibu wa huduma za tiba mkoa wa Manyara Elford  Mukerebe wakati akiongea na fm Manyara, amesema daliliza za ugonjwa huo ni pamoja na homa kali ya ghafla, kulegea kwa mwili, maumivu ya misuli, kuumwa kichwa, vidonda kooni, kutapika, kuhara , vipele kwenye ngozi, na kutokwa damu sehemu za wazi .

sauti ya mratibu wa huduma za tiba mkoa wa Manyara Elford  Mukerebe

Kwa upande wake afisa afya mkoa wa manyara Suten Mwabulambo,amewataka wananchi kuepuka kugusa maiti ya mtu aliyekufa kwa dalili za ugonjwa huo,kuepuka kutumia nguo, na vyombo vilivyotumiwa na mtu mwenye dalili hizo  na akiwahimiza wananchi kuzingatia usafi kwa kunawa mikono kwa maji  safi na salama.

sauti ya afisa afya mkoa wa manyara Suten Mwabulambo