FM Manyara

DC Babati kushugulika na wadaiwa sugu Ankara za maji

11 November 2025, 7:13 pm

picha ya Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emmanuela Kaganda

Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emmanuela Kaganda, ameziagiza taasisi za umma zikiwemo shule, zahanati na vituo vya afya ambavyo ni wadaiwa sugu wa ankara za maji, kulipa madeni yao mara moja kabla ya kuanza msako. Hatua hiyo inalenga kuhakikisha uendelevu wa upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi.

Na Mzidalfa Zaid

Agizo hilo limetolewa katika mkutano mkuu wa nusu mwaka wa vyombo vya watoa huduma za maji ngazi ya jamii wilayani Babati, baada ya RUWASA kutoa taarifa ya malimbikizo ya zaidi ya shilingi milioni 19 kutoka kwa watumiaji.

sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emmanuela Kaganda,

Meneja wa RUWASA Wilaya ya Babati, Mhandisi Hubert Kijazi, amebainisha kuwa wadaiwa wakubwa ni shule za msingi na sekondari, pamoja na vituo vya afya, na tayari taasisi hizo zimekumbushwa kulipa madeni hayo.

sauti ya Meneja wa RUWASA Wilaya ya Babati Mhandisi Hubert Kijazi

Viongozi wa Jumuiya za Watumiaji Maji wamesisitiza umuhimu wa malipo kwa wakati ili kuepusha kukwama kwa shughuli za uendeshaji, ikiwemo kulipia huduma ya umeme kwa pampu za maji.

sauti ya Viongozi wa Jumuiya za Watumiaji Maji

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Manyara James Kionaumela, hali ya upatikanaji wa maji mkoani imefikia asilimia 78.9, huku Babati ikifikia asilimia 80.9.

sauti ya Meneja wa RUWASA Mkoa wa Manyara James Kionaumela