FM Manyara

EWURA  yawataka wananchi kutumia nishati safi ya kupikia

12 December 2025, 5:11 pm

Picha ya Meneja wa Ewura kanda ya Kaskazini kaskazini Lorivii Long’idu(kulia)

Wananchi mkoani Mayara na kanda ya kaskazini kwa ujumla wametakiwa kutumia nishati safi ya kupikia ili kulinda mazingira kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi hapa nchini.

Na Mzidalfa Zaid

Wito huo umetolewa leo na Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) kanda ya kaskazini Lorivii Long’idu wakati akiongea na Fm Manyara, amesema matumizi ya nishati ambayo sio safi yamekuwa yakileta changamoto katika afya.

Sauti ya Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) kanda ya kaskazini Lorivii Long’idu

Amesema wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi kutumia nishati safi ya kupikia, ambapo kwa sasa muitikio ni mzuri kutokana  na jamii kuwa na uelewa.