FM Manyara
FM Manyara
22 May 2026, 7:44 pm

Kampuni ya simu za mikononi ya Yas na Mixx by Yas Tanzania wamezindua mnara wa mawasiliano wenye uwezo wa 4G plus kwenye kijiji cha Gendabi Wilayani Hanang Mkoani Manyara.
Na Marino Kawishe
Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho Kiongozi wa Kanda ya Kaskazini kutoka mtandao huo Robert Sanyagi amesema lengo la Kampuni ya Yas na Mixx by Yas Tanzania nikufikisha huduma bora za mtandao kwa jamii na hasa maeneo ambayo yanachangamoto kubwa za mawasiliano.

Aidha Meneja wa mtandao wa Yas Tanzania Mkoani Manyara Ladislaus Karo amesema kufwatia changamoto ya kijiji cha Gendabi kukumbwa na maporomoko ya matope mwaka 2023 walifanya utafiti nakugundua eneo hilo lina shida ya mtandao nakuona Kuna haja yakuweka mnara kwenye eneo hilo.
Nao wananchi wa kijiji hicho wameishukuru Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Yas Tanzania kwakuwaletea mnara huo ambao utatoa huduma za internet na kuwasiliana baina ya wananchi hao na maeneo mengine.
Uzinduzi wa mnara huo ni muendelezo wa miradi ya kampuni hiyo ambayo imewekeza zaidi ya sh Trillion 1kwenye huduma za mawasiliano hapa nchini Tanzania na kuwa kampuni yenye minara zaidi ya elfu 4800 mpaka sasa.

