FM Manyara
FM Manyara
7 July 2026, 3:10 pm

Picha ya Kaimu mkuu wa wilaya ya Babati Remidius Mwema
Wilaya ya Babati inatarajia kuupokea Mwenge wa Uhuru July 14 2026 ukitokea Wilaya ya Kiteto, ambapo utakagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi 14 ya maendeleo iliyopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati na Halmashauri ya Mji wa Babati.
Na Mzidalfa Zaid
Hayo yameelezwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Babati ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Remidius Mwema amesema maandalizi ya kuupokea Mwenge wa Uhuru yamekamilika kwa kiwango cha kuridhisha.
Amesema Mwenge wa Uhuru utapokelewa rasmi katika Kata ya Galapo kabla ya kuanza ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Mji wa Babati, Martin Petro, amesema baadhi ya maeneo yametengwa kwa ajili ya mbio za Mwenge kwa miguu ili kutoa fursa kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli hiyo.
Aidha amesema July 12, 2026 kutafanyika kongamano la vijana litakalowakutanisha vijana kutoka maeneo mbalimbali kujadili masuala ya uzalendo, maendeleo na fursa zinazowahusu.

Nae mratibu wa mwenge wa Uhuru halmashauri ya wilaya ya Babati James David , amewataka wananchi wote wa halmashauri ya wilaya hiyo kujitokeza kwa Wingi maeneo ambayo mwenge wa uhuru utapita .
