FM Manyara

RC Sendiga azindua majiko banifu

11 November 2025, 5:12 pm

Picha ya mkuu wa mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, amezindua rasmi mradi wa uuzaji na usambazaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku mkoani Manyara ambapo Uzinduzi huu ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa upatikanaji na uhamasisha wa matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia.

Na Mzidalfa Zaid

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,  Sendiga amesema mpango huo umelenga kuhakikisha wananchi wote, hususani wa kipato cha chini, wanapata fursa ya kutumia nishati safi na salama ya kupikia kwa gharama nafuu na amewaagiza Wakuu wa Wilaya wote mkoani Manyara kusimamia kwa makini zoezi hili, ili kuhakikisha majiko hayo yanauzwa kwa bei iliyoelekezwa na kuepuka udanganyifu wa aina yoyote unaoweza kujitokeza wakati wa zoezi.

sauti ya mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga

Uzinduzi huu umefanyika katika Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Manyara iliyopo wilaya ya Babati, ambapo jumla ya majiko banifu 7,914 yatauzwa na kusambazwa kwa bei ya ruzuku ya kiasi cha TZS 11,200 ambayo ni sawa na aslimia 80 ya ruzuku ya TZS 56,000 ambayo ni bei ya awali ya jiko.x

Aidha, Kampeni Hiyo  ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan za kupunguza uharibifu wa mazingira unaosababishwa na matumizi makubwa ya kuni na mkaa na pia kulinda afya za wananchi.