FM Manyara

RC Sendiga aamuru bar kufungwa kwa kutiririsha majitaka

12 December 2025, 10:31 pm

Picha ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga pamoja na viongozi wa idara mbalimbali wakikagua Maji taka yakipitishwa kwenye mtaro.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga amefanya ziara ya kushtukiza kwenye Bar ya Barazani inayotiririsha maji machafu aina ya kinyesi cha binadamu na kumwamuru mkuu wa wilaya ya Babati na OCD kuifunga Bar hiyo mpaka mmiliki wake atakapojisalimisha mwenyewe ofisini kwake.

Na Mzidalfa Zaid

Sendiga ametoa agizo hilo katika mwendelezo wa ziara yake, ambapo amefika katika bar hiyo na kujionea namna maji machafu yanavyoingia kwenye makazi ya watu.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga

Awali afisa mazingira halmashauri ya mji Babati ameeleza kuwa mmiliki wa eneo hilo amekuwa akikaidi taarifa za afisa mazingira wa halmashauri ya mji wa Babati za kutakiwa kufanya usafi katika mazingira hayo.

Aidha , hatua hiyo ya mkuu huyo wa mkoa kufika katika bar hiyo ni baada ya kupigiwa simu na wananchi wa eneo hilo asubuhi ya Leo wakilalamikia changamoto hiyo.