FM Manyara

Wawekezaji watakiwa kuchangamkia fursa Manyara

5 May 2026, 7:14 pm

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga kushoto, na baadhi ya wawekezaji kulia

Wawekezaji  mkoani Manyara wametakiwa kuchangamkia fursa ya kuwekeza biashara mbalimbali  ili kujiinua kiuchumi  baada  ya Geti la Mamire  kufunguliwa  kwa ajili ya  kupitisha  magari  ya watalii.

Na Mzidalfa Zaid

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga  ameyasema hayo leo wakati akiongea katika kikao cha kamati ya uwekezaji mkoa wa Manyara , amesema serikali imefanikisha  kufungua geti hilo, hivyo   kunapofunguliwa biashara mbalimbali itasaidia wawekezaji kupata huduma muhimu na kukuza uchumi wa mkoa wa Manyara.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga  

Kwa upande wake afisa biashara mkoa wa Manyara Ally Mokiwa ,amesema  mkoa wa Manyara una jumla ya wawekezaji  138 ambapo jitihada mbalimbali  zinaendelea za kuweka  mazingira bora na kuvutia uwekezaji.

Sauti ya afisa biashara mkoa wa Manyara Ally Mokiwa
Picha ya afisa biashara mkoa wa Manyara Ally Mokiwa

Akiwasilisha ripoti ya tiseza , Katibu wa kamati ya uwekezaji mkoa ambae pia ni kamanda wa uhamiaji mkoa Philon Phabian Kyetema amesema kiwango Cha miradi ya upanuzi kinazidi kuongezeka katika mkoa wa Manyara.

Sauti ya Katibu wa kamati ya uwekezaji mkoa ambae pia ni kamanda wa uhamiaji mkoa Philon Phabian Kyetema