FM Manyara

Sendiga afungua maonesho ya mbolea duniani mkoani Manyara

10 October 2024, 9:31 pm

Picha ya mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya siku ya mbolea duniani

Maonyesho ya mbolea yakiwa yamefunguliwa rasmi Leo 10,october 2024, mkoani Manyara  mkuu wa mkoa wa manyara amewataka wafanyabiashara kusogeza mbolea kwa wananchi kwa kifungua ofisi za wakala vijijini ili kuwapunguzia gharama za kufuata  mbolea mijini.

Na George Augustino.

Mkuu wa mkoa wa manyara Queen Sendiga amewaagiza wenyeviti pamoja na kamati za pembejeo za wilaya za mkoa wa manyara kuhakikisha wananchi na wakulima wote kwenye maeneo yao wanajiandikisha pamoja na kuhuisha taarifa zao ili  wanufaike na mbolea za ruzuku.

Sendiga ameyasema hayo leo 10,October 2024 alipokuwa akifungua maonesho ya siku ya mbolea duniani yanayofanyika kitaifa mkoani manyara na kilele chake ikiwa ni October 13 mwaka huu, amesema wafanyabiashara wanawajibu wa kusogeza mbolea kwa wananchi kwa kufungua ofisi za uwakala vijijini ili kuwapunguzia wakulima gharama za kufuata mbolea mijini.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa manyara

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya udhibiti wa mbolea tanzania Joel Laurent amesema katika maonesho  hayo kutakuwa na makampuni ya mbolea, taasisi pamoja na wadau wengine ambao wataonesha huduma mbalimbali katika mnyororo wa thamani wa mbolea, na wananchi kupata elimu sahihi ya matumizi ya mbolea 

Sauti ya mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya udhibiti wa mbolea tanzania

Aidha, mwenyekiti wa bodi ya TFRA Antony Diallo amesema mamlaka ya udhibiti wa mbolea  imekuwa ikihakikisha wakulima nchini wanapata na kutumia mbolea bora kwa wakati kwa bei himilivu pamoja na kutoa elimu kwa wakulima licha ya jukumu lao la kudhibiti biashara ya mbolea hapa nchini.

Sauti ya mwnyekiti wa bodi ya mamlaka ya udhibiti wa mbolea tanzania