FM Manyara
FM Manyara
9 September 2024, 7:39 pm

Ikiwa imebaki siku moja kukamilika kwa zoezi la uboreshaji wa taarifa katika daftari ka kudumu la mpiga kura, mkuu wa wilaya ya Babati amewataka wananchi kufika katika vituo vilivyopangwa
Na George Agustino
Wananchi wilayani Babati mkoani Manyara wametakiwa kufika katika vituo vilivyopangwa kwa ajili ya kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la mpiga kura ili kutimiza haki zao za kikatiba za kuchagua viongozi wanao wahitaji katika uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa utakao fanyika november mwaka huu na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani.
Wito huo umetolewa leo na mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda alipofika kuboresha taarifa zake katika kituo cha shule ya sekondari Kwaraa Kilichopo wilayani Babati mkoani Manyara.
Amesema yeye kama kiongozi ameungana na wananchi wengine kutumiza haki hiyo yakikatiba ambapo amewataka wananchi wengine ambao bado hawajajiandikisha au kuhakiki taarifa zao kushiriki zoezi hilo kwakua zoezi hilo linahitimishwa september 10 mwaka huu.
Kwa upande wake mkuu wa shule ya sekondari Kwaraa Deogratius Michae amewahimiza wanafunzi wa shule hiyo ambao wamefikisha umri wa kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura kujiandikisha kila mmoja katika mtaa wake anaoishi ili wasikose haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaotaka na kuwaletea maendelea.