FM Manyara
FM Manyara
1 May 2026, 8:32 pm

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga , amewataka wafanyakazi kutumia nishati safi ya kupikia kwa kutumia majiko ya umeme ambayo yanatumia umeme kidogo na kuivisha kwa muda mfupi.
Na Mzidalfa Zaid
Amesema hayo Leo katika siku ya wafanyakazi(meimosi) mkoani Manyara baada ya kutembelea banda la TANESCO ambapo amesema Lengo la serikali ni Kuhakikisha wananchi wanaachana na matumizi ya nishati chafu ya kupikia.
Kwa upande wake Meneja wa Tanesco mkoa wa Manyara Regina Mvungi, amesema tanesco inauza majiko kwa wananachi kwa gharama nafuu ili Kila mwananchi aweze kunufaika Kwa kulipia kidogo kidogo.
