FM Manyara

Japani yafadhili Madarasa, vyoo na Madawati Orngadida

2 July 2026, 7:53 pm

Picha ya Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daniel Sillo

Zaidi ya shilingi Milion 300 ambazo kwa asilimia mia moja zimefadhiliwa na Serikali ya Japan kupitia Ubalozi wake hapa Nchini  zimetumika kukamilisha miradi ya ujenzi wa madarasa matatu, vyoo vya wanafunzi na waalimu  pamoja na madawati katika shule ya msingi Orngadida  iliyopo kata ya Qash wilaya ya Babati mkoani Manyara. 

Akizungumza mbele ya mgeni rasmi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daniel Sillo na wananchi wa kata ya Qash Meneja mkazi wa Shirika la So They Can Tanzania Roselyne Mariki amesema mradi huo umefanikishwa kwasababu ya mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Shirika hilo na Serikali ya Japan.

Sauti ya Meneja mkazi wa Shirika la So They Can Tanzania

Akikabidhi mradi huo kwa niaba ya Balaozi wa Japani Tanzania Hashimoto Jin amesema wanaamini mradi huo utawanufaisha watoto wa Manyara na Tanzania kwa ujumla. 

Sauti ya Mwakilishi wa balaozi wa Japani nchini Tanzania

Aidha mgeni Rasmi Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwenye hafla hiyo Daniel Sillo ameishukuru Serikali ya japani kwa ushirikiano wanaotoa kwenye miradi mbali mbali huku akisema mazing bora ya Uwekezaji ndio yanayochochea maendeleo kwa serikali ya Rais Samia Hassan.

Sauti ya Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania

Nae Katibu tawala wa Mkoa wa Manyara Mariam Muhaj Akizungumza na wananchi wa kata ya Qash amewataka kulinda miundo mbinu iliyojengwa kwani inaenda kuwakomboa na changamoto kubwa iliyokuwepo hapo awali.

Sauti ya Katibu tawala wa mkoa wa Manyara

Mradi huo wa Madarasa matatu na matundu 25 ya vyoo pamoja na madawati 60 kila Darasa na ujenzi wa kisima cha maji umekamilika kwa asilimia mia moja na utaanza kutumika baada ya shule kufunguliwa kwa muhula wa pili mwezi huu wa saba.