FM Manyara
FM Manyara
12 December 2025, 7:49 pm

Wakati wananchi wakiwa katika maandalizi ya sikuu za mwisho wa mwaka , Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Manyara, imewataka wananchi mkoani humo kuadhimisha sikukuu hizo kwa kukataa Rushwa.
Na Mzidalfa Zaid
Wito huo umetolewa leo na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Manyara Bahati Haule, wakati akiongea na Fm Manyara, amesema kila mwananchi anapaswa kuwa mstari wa mbele kupinga vitendo vya Rushwa.
Aidha, amewataka wananchi kudumisha utawala bora na utawala wa sheria , kuhifadhi amani, haki na utulivu pamoja na kulinda mali na raslimali za Taifa.