FM Manyara
FM Manyara
30 July 2026, 6:44 pm

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kaskazini imekutana na wadau wa sekta ya nishati na maji Kanda ya kaskazini kwa lengo la kuwakumbusha majukumu yao ya kazi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Na Mzidalfa Zaid
Akizungumza katika kikao hicho, Meneja wa EWURA Kanda ya Kaskazini, George Mhina, ameziagiza mamlaka za maji kushughulikia changamoto zinazowakabili wananchi, ikiwemo ankara zisizoendana na matumizi halisi ya maji.
Kwa upande wa sekta ya nishati, Mhina ameielekeza TANESCO kuhakikisha wananchi wanaokidhi vigezo wanaunganishiwa huduma ya umeme kwa wakati.


Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano ya Umma wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga, Bi. Devotha Mayala, amesema mafunzo hayo yamewapa uelewa zaidi kuhusu namna bora ya kuwahudumia wananchi na kushughulikia changamoto zinazojitokeza katika utoaji wa huduma.
Nae Afisa Uhusiano wa TANESCO Mkoa wa Manyara, Bw. Samweli Mandari, ameipongeza EWURA kwa kuandaa mafunzo hayo, akisema yatasaidia kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi na kuboresha huduma kwa wananchi wa sekta za maji na nishati.
