FM Manyara

Babati DC yazindua chanjo ya polio

28 August 2026, 6:09 pm

Picha ya kaimu mkuu wa wilaya ya Babati akimpa chanjo ya polio mtoto chini ya miaka 10

Halmashauri ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara imezindua rasmi zoezi la utoaji wa chanjo ya polio kwa watoto chini ya Miaka 10 zoezi balo limeanza jana katika maeneo mbalimbali ya halmashauri hiyo.

Na Mzidalfa Zaid

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Babati, Remidius Mwema, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo katika kata ya Magugu, amewataka wazazi na walezi kuitikia zoezi hilo kwa kuwapeleka watoto wao kupata chanjo ya polio ili kuwalinda dhidi ya ugonjwa huo ambao unaweza kusababisha ulemavu.

Sauti ya Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Babati, Remidius Mwema

Mwema amesisitiza umuhimu wa wazazi kutoa ushirikiano kwa wahudumu wa afya wanaofika katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha watoto wote wanaostahili chanjo wanapata huduma hiyo.

Kwa upande wake, Mratibu wa Chanjo wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, James Mleli, amesema zaidi ya watoto 160,000 wanatarajiwa kufikiwa na chanjo ya polio katika halmashauri hiyo.

Sauti ya Mratibu wa Chanjo wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, James Mleli
Sauti ya Mratibu wa Chanjo wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, James Mleli

Amesema lengo ni kuhakikisha kila mtoto anayestahili anapata chanjo hiyo kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa polio.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Anna Mbogo, amesema zoezi la utoaji wa chanjo linafanyika katika maeneo mbalimbali ikiwemo nyumba kwa nyumba, shuleni na maeneo ya mikusanyiko ya watu, ili kuwafikia watoto wengi zaidi.

Ameongeza kuwa wazazi na walezi wanapaswa kutumia fursa hiyo kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo kwa wakati.

Sauti ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Anna Mbogo
Picha ya baadhi ya wanafunzi wakisubiria kupata chanjo ya polio