FM Manyara

Babati mji yaongoza utoaji wa chanjo ya polio

28 August 2026, 4:25 pm

Picha ya uzinduzi wa chanjo ya polio Babati mji

Halmashauri ya mji wa Babati imefanikiwa kuwapa chanjo ya polio ya matone watoto zaidi ya elfu 21 kwa siku ya kwanza ya kampeni hiyo iliyoanza rasmi jana august 27 mwaka 2026.

Na Marino Kawishe

Akifungua rasmi zoezi la chanjo kwa halmashauri ya mji  wa Babati leo august 28 mwaka 2026  kaimu mkuu wa wilaya ya Babati Remidius Mwema amewataka wananchi kuendelea kuwapeleka watoto kwenye maeneo yote ambayo chanjo hiyo inatolewa ili kufikia malengo kwa halmashauri hiyo

Kwa upande wake mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Babati  Nassibu Msuya akitoa takwimu kwa siku ya kwanza ya zoezi hilo amesema mwitikio umekuwa mkubwa na hali ikiendelea hiyo watoto wote elfu 38249 watafikiwa kwenye zoezi hilo la kampeni ya chanjo ya polio kama ilivyokadiriwa.

Sauti ya mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Babati  Nassibu Msuya

Akizungumza na fm Manyara  Mwakilishi kutoka Wizara ya afya na msimamizi wa  zoezi la utoaji chanjo ya polio kwa matone kwa watoto walio chini ya umri wa miaka kumi Mkoani Manyara Dr Mwendwa   Mwenesi amesema lengo lililowokwa na wizara litafikiwa iwapo ushirikiano utaenda baina ya serikali na wananchi wote.

Zoezi la kampeni ya chanjo ya polio kwa njia ya matone limeingia siku ya pili leo ambapo mkoa wa Manyara tayari umechanja watoto chini ya miaka kumi kwa asilimia 46 hadi sasa huku halmashauri ya mji ikiwa kinara  kwa asilimia 56.3 ikifwatiwa na halmashauri ya wilaya ya Babati.