FM Manyara

Vipimo vya DNA vya mkutanisha mtoto na Mama yake Manyara

16 September 2026, 9:56 pm

Picha ya mkuu wa mkoa wa Manyara Martin Shigela akikabidhi mtoto aliyepotea kwa mama yake

Uongozi wa ofisi ya mkoa wa Manyara umekabidhi Mtoto aliyepotea mkoani shinyanga kwa mama yake baada ya kutelekezwa Manyara

Na Emmy Peter

Mtoto aliyekuwa akijulikana kwa jina la Stanley, ambaye awali aliripotiwa kupotea, amepatikana na kuunganishwa na mama yake mzazi baada ya vipimo vya vinasaba (DNA) kufanyika kupitia Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

Majibu yaliyotolewa na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali yameonesha kuwa mtoto huyo ni mtoto halali wa mwanamke aliyedai kuwa mama yake mzazi, Mtoto huyo ametajwa kwa jina la Fadhili Eliasu na anatoka Kahama, Mkoa wa Shinyanga.

Aidha, Mama mzazi wa mtoto huyo ameeleza kuwa mtoto alipotea wakati akiwa katika eneo la soko, ambapo alimuacha kwa muda akienda kufanya shughuli zake. Aliporudi, aligundua kuwa mtoto hakuwepo na kuanza kumtafuta kwa kuwauliza watu waliokuwa eneo hilo.

Sauti ya Mama mzazi wa mtoto aliyepotea

Kwa upande wake Mkuuu wa Mkoa wa Manyara Martin shigela Amemshukuru ofisi ya Mkemi Mkuuu wa Maji hayo na kimshukuru glory Lazaro ambaye alikuwa Mlezi wa Mtoto ambapo Ametoa wito kwa jamiii kuendelea kutunza Watoto na kuacha tabia ya kutupa watoto .

Sauti ya Mkuuu wa Mkoa wa Manyara Martin shigela
Picha ya mkuu wa mkoa wa Manyara Martin Shigela akikabidhi mtoto aliyepotea kwa mama yake