FM Manyara
FM Manyara
15 September 2026, 12:54 pm

Mkoa wa Manyara kupitia idara ya afya imechukua tahadhari za kukabiliana na magonjwa ya mlipuko yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua za elinino
Na Mzidalfa Zaid
Kufuatia utabiri wa mvua za El Niño katika maeneo mbalimbali nchini, Idara ya Afya mkoani Manyara imechukua tahadhari za kukabiliana na magonjwa ya mlipuko yanayoweza kujitokeza kutokana na mafuriko.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Andrew Method, amesema tayari wameunda kamati maalumu ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ili kuhakikisha mkoa unakuwa tayari kukabiliana na changamoto zitakazoweza kujitokeza.
Dkt. Method amewataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kuzingatia kanuni za afya, ikiwemo kunywa maji yaliyochemshwa na kunawa mikono mara kwa mara, huku akisema idara hiyo inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko.
Kwa upande wake afisa afya Kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Manyara Suten Mwabulambo amezungumzia team ambayo ipo tayari iwapo kutatokea changamoto yoyote inayohusiana na mvua zinazotarajiwa kuanza kati ya mwishoni mwa September na mwanzoni mwa October mwaka huu.
