FM Manyara
FM Manyara
1 October 2026, 3:38 pm

Kliniki ya Ardhi inaendelea mkoani Manyara katika Viwanja vya Tanzanite Kwaraa ikiwa zimebakiza siku chache kufikia tamati ambapo Kliniki hiyo inalenga kusogeza huduma muhimu za ardhi karibu na jamii.
Na Mzidalfa Zaid
Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kufika katika viwanja wa Tanzanite Kwaraa katika klininik ya ardhi inayoendelea kwa Lengo la kutatua kero mbalimbali za ardhi.
Akizungumza kuhusu klinik hiyo Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Manyara Erick Makundi, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika siku hizi chache zilizosalia ili kutumia fursa hiyo adhimu.
Wananchi wanaotembelea viwanja hivyo wanapatiwa elimu ya sheria za ardhi, utoaji wa ankra na ukusanyaji wa kodi ya pango la ardhi, pamoja na kusikiliza na kutatua migogoro na changamoto zote za umiliki zinazowakabili kwa muda mrefu ambapo baadhi yao wameelezea namna walivyonufaika na klinik hiyo.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia Ofisi ya Ardhi ya Mkoa wa Manyara ilianzisha huduma hiyo tangu tarehe Septemba 22 na inatarajiwa kuhitimishwa rasmi tarehe 03 Oktoba 2026 yenye kauli mbiu isemayo “Ardhi ni mtaji, itunze ikutunze.