FM Manyara

Wananchi Manyara watahadharishwa matumizi holela ya dawa

19 November 2026, 5:58 pm

Picha ya  Mfamacia kutoka hospital ya Rufaa Manyara Amos Nzungu 

Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kutunza na kutumia dawa kwa kufuata ushauri unaotolewa na wataalam wa afya ili kupunguza changamoto ya usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa .

Na Marino Kawishe

Inakadiriwa  kati  ya vifo  elfu 10 hadi elfu 50  nchini Tanzania  vinatokana na usugu wa vimelea  vya magonjwa  dhidi ya dawa.

Hayo yamesemwa leo na mfamasia kutoka hospital ya rufaa  ya mkoa wa Manyara Amos Nzungu, wakati  akizungumza  na fm Manyara kwenye kipindi cha mseto wa leo,  ametaja sababu moja wapo  za usugu wa dawa  ni pamoja na matumizi holela ya dawa bila kufuata utaratibu wa wataalamu wa afya.

Sauti ya mfamasia kutoka hospital ya rufaa  ya mkoa wa Manyara Amos Nzungu

Aidha  katika maadhimisho ya wiki  usugu  wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa watoa huduma wameaswa kufuata  miongozo  ya kimatibabu iliyokubalika kisheria ili kusaidia kupunguza matumizi holela ya dawa kwa binadamu.