FM Manyara
FM Manyara
17 October 2026, 11:49 pm

Kampuni ya Mati Super Brands Ltd imeshiriki na kudhamini kwa mara nyingine Maonesho ya Nne ya Kibiashara ya Tanzanite Manyara Trade Fair 2026 kupitia bidhaa zake, ikiwemo kinywaji cha Strong Dry Gin.
Na Mzidalfa Zaid
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonesho hayo, Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Isack Piganio, amesema ushiriki wao unalenga kupanua soko la bidhaa za kampuni hiyo, pamoja na kuwapa wafanyabiashara na wadau mbalimbali fursa ya kujenga mahusiano ya kibiashara na kutafuta masoko mapya.
Amewataka wananchi kutembelea banda la Mati Super Brands Ltd ili kujionea bidhaa mbalimbali zinazopatikana, zikiwemo vinywaji changamshi vinavyotolewa na kampuni hiyo.

Maonesho hayo yamezinduliwa rasmi Oktoba 17, 2026, katika viwanja vya Tanzanite Kwaraa, Babati, mkoani Manyara, na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati, CPA Shaaban A. Mpendu, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Martine Shigela.
