FM Manyara

Serikali yaombwa kutenga bajeti ya kilimo cha asili

6 November 2026, 5:24 pm

Picha ya baadhi ya washiriki wa semina ya uchambuzi wa bajeti yenye mrengo wa kijinsia

Licha ya Jitihada kubwa inayotolewa na mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP kukuza kilimo cha mbegu za asili bado inaonekana eneo la kilimo cha mbegu za asili halipewi msukumo mkubwa kwenye Bajeti za serikali za kila mwaka.

Na Marino Kawishe

Imeelezwa kuwa kilimo cha mbegu za asili bado inaonekana eneo la kilimo cha mbegu za asili halipewi kipaumbele, ambapo serikali imeombwa kutenga bajeti ya kilimo hicho.

Akitoa tathimini ya mafunzo ya uchambuzi wa bajeti yenye mrengo wa kijinsia yaliyoandaliwa na mtandao wa Jinsia Tanzania na kuhudhuriwa na wadau mbali na wajumbe wa vikundi vya taarifa na maarifa  kutoka halmashauri ya wilaya ya Babati na mbulu TC,mkufunzi wa mafunzo hayo Dr  Godfrey Chambua amesema kuwa elimu inapaswa kuendelea kutolewa kwa maeneo mengi zaidi.

Sauti ya mkufunzi wa mafunzo hayo Dr  Godfrey Chambua

Aidha baadhi ya washiriki waliotoa maoni yao wamesema zipo changamoto ambazo ndani ya miaka mitatu ya mradi huo zimekuwa kikwazo kufikia malengo ikiwemo kutokutengewa bajeti za kutoa elimu ya kilimo cha mbegu za asili na kukosekana kwa muitikio kwa baadhi kwenye nafasi ya mwanamke na uongozi.

sauti ya baadhi ya washirki

Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Babati mkoani Manyara Anna Mbogo ametoa wito kwa jamii kuhakikisha masuala ya ukatili yanaendalea kupewa kipaumbele na kuwap nafasi watoto kusema yalewanayokabiliana nayo.

Sauti ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Babati mkoani Manyara Anna Mbogo

Mafunzo hayo yamewakutanisha baadhi ya wadau wakimo kutoka idara ya uchumi, maendeleo ya jamii, kilimo na wajumbe kutoka vituo vya taarifa na maarifa vya mamire na Murray mkoani Manyara. 

Picha ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Babati mkoani Manyara Anna Mbogo