FM Manyara
FM Manyara
26 November 2026, 9:34 am

Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kutoa taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyotokea katika maeneo yao, kulinda watoto dhidi ya ukatili pamoja na kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kudhibiti vitendo hivyo.
Na Mzidalfa Zaid
Wito huo umetolewa leo na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Manyara, Johannes Kerya, alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia mkoani Manyara, uliofanyika katika Soko Kuu la Babati.

Katika uzinduzi huo kumehudhuriwa na wananchi mbalimbali pamoja na viongozi mbalimbali wakiwmo maafisa ustawi wa jamii ,dawati la jinsia pamoja na maaskari wa jeshi la polisi .