FM Manyara
FM Manyara
27 October 2026, 11:21 pm

Shirika la Farm Africa limewakutanisha wakulima kutoka mikoa ya Manyara, Morogoro na Singida na kuwapatia elimu kuhusu matumizi sahihi ya mbegu bora kwa lengo la kuongeza tija katika shughuli za kilimo.
Na Mzidalfa Zaid
Wakulima kutoka mikoa ya Manyara, Singida na Morogoro wamepatiwa mafunzo juu ya matumizi ya mbegu Bora kuanzia uandaaji.
Akizungumza baada ya mafunzo hayo, Afisa Ufuatiliaji na Tathmini wa mradi kutoka shirika la Farm Africa, Godson Lema, amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuwajengea wakulima uwezo wa kuandaa na kutumia mbegu bora, pamoja na kuwasaidia kuepukana na changamoto zinazotokana na matumizi ya mbegu duni.

Kwa upande wake, Mkaguzi kutoka Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) Makao Makuu, Frank Faida, amesema kuwa wakulima wamepewa elimu ya namna ya kutambua mbegu bora ili waweze kufanya maamuzi sahihi wakati wa kununua na kutumia mbegu kwa ajili ya shughuli zao za kilimo.
Baadhi ya wakulima walioshiriki mafunzo hayo wamelishukuru shirika la Farm Africa kwa kuwawezesha kupata elimu hiyo, wakieleza kuwa maarifa waliyoyapata yatawasaidia kuboresha shughuli zao za kilimo na kuongeza uzalishaji wenye tija.