FM Manyara
FM Manyara
22 October 2026, 7:39 pm

Kamati ya Usalama Barabarani mkoani Manyara imekabidhi gari kwa Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa lengo la kurahisisha utendaji kazi wa jeshi hilo katika kusimamia sheria za usalama barabarani.
Na Mzidalfa Zaid
Katika kuhakikisha jeshi la polisi linaendelea kusimamia Sheria za usalama barabarani , kamati ya usalama barabarani mkoa wa Manyara imekabidhi gari kwa jeshi la polisi.
Akizungumza baada ya kukabidhi gari hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani mkoani Manyara, Emmanuel Mollel, amesema hatua hiyo inalenga kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya jeshi la polisi, hususan katika kusimamia sheria za usalama barabarani kwa wakati.
Kwa upande wake, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Manyara, Johannes Kerya, amesema kupatikana kwa gari hilo kutasaidia kuongeza nguvu katika operesheni za kukabiliana na madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarani.