FM Manyara

Kampeini ya nishati safi ya kupikia yauza majiko 21 Mbulu

10 October 2026, 5:34 pm

Picha ya baadhi ya watumishi wa TANESCO mkoa wa Manyara wakiwakabidhi wateja majiko ya nishati safi ya kupikia

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Manyara limeuza majiko 21 ya umeme kwa wananchi wa Mbulu Mjini kupitia kampeni ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia yenye kaulimbiu ya “Pika Kijanja, Pika kwa Umeme.”

Na Mzidalfa Zaid

Wananchi wilayani Mbulu mkoani Manyara wameendelea kunufaika na kampeini ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kununua majiko ya kisasa ya. Nishati safi.

Kampeni hiyo imefanyika  katika viwanja vya Soko la Mbulu Mjini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja 2026 yenye kaulimbiu ya “Extra Mile,” ambapo wananchi wamepata elimu kuhusu matumizi salama na yenye ufanisi ya umeme, hususan katika shughuli za kupikia.

Akizungumza wakati wa kampeni hiyo, Afisa Uhusiano wa TANESCO Mkoa wa Manyara, Samuel Mandari, amesema elimu hiyo inalenga kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu faida za kutumia umeme kupikia, matumizi bora ya nishati na usalama wa vifaa vya umeme majumbani na kwenye biashara.

Picha ya watumishi wa TANESCO wakiwa na majiko ya nishati safi

Meneja wa TANESCO mkoa wa Manyara Regina Mvungi amesema Kampeni hiyo imeambatana na burudani kutoka kwa wasanii na ma-DJ, huku TANESCO ikiendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa lengo la kulinda afya za wananchi, kutunza mazingira na kuunga mkono jitihada za Taifa za kuhamia kwenye matumizi ya nishati safi na endelevu.

Sauti ya Meneja wa TANESCO mkoa wa Manyara Regina Mvungi
Picha ya meneja wa TANESCO mkoa wa Manyara Regina Mvungi akikabidhi jiko la nishati safi ya kupikia kwa mwananchi .