FM Manyara

Maonyesho ya Tanzanite Manyara trade fair yazinduliwa rasmi

17 October 2026, 11:25 pm

Picha ha mgeni rasmi ambae ni mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Babati akiaambatana na viongozi mbalimbali

Maonyesho ya Tanzanite Manyara Trade Fair yamezinduliwa rasmi leo katika viwanja vya stendi ya zamani, Babati, yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wananchi kutoka maeneo tofauti.

Na Mzidalfa Zaid

Wananchi mbalimbali kutoka maeneo mbalimbali wamehudhuria Katika uzinduzi wa maonyesho ya Tanzanite Manyara trade fair ambayo yamezinduliwa rasmi Leo na kilele chake kikitarajiwa kuwa October 21 mwaka huu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati, Shaaban Mpendu, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Martin Shigela, amewataka wananchi kutumia fursa ya maonyesho hayo kutangaza biashara zao, kujitangaza na kununua bidhaa mbalimbali zinazopatikana katika maonyesho hayo.

Sauti ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Babati, Shaaban Mpendu,

Mpendu amesema maonyesho hayo ni fursa muhimu kwa wafanyabiashara na wajasiriamali kukuza shughuli zao za kiuchumi, kutangaza bidhaa na huduma wanazozalisha pamoja na kupata wateja wapya.

Picha ya mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Babati Shaaban Mpendu

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara Mkoa wa Manyara, Mussa, amesema maonyesho hayo yamekuwa yakitoa fursa kwa wafanyabiashara kukuza biashara zao, kubadilishana uzoefu na kupanua mitandao ya masoko.

Sauti ya Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara Mkoa wa Manyara, Mussa,

Naye Meneja wa Chemba ya Taifa ya Biashara Mkoa wa Manyara, Lerunde Laizer, amesema wameweka mikakati mbalimbali ya kuendeleza maonyesho hayo, ikiwemo kupata eneo maalumu kwa ajili ya maonyesho na kuanzisha maonyesho ya kimataifa yatakayosaidia kupanua wigo wa biashara na kuvutia wadau wengi zaidi.

Sauti ya Meneja wa Chemba ya Taifa ya Biashara Mkoa wa Manyara, Lerunde Laizer
Mgeni rasmi akikagua mabanda