FM Manyara
FM Manyara
24 September 2026, 7:42 pm

Shirika la Biashara na Haki za Binadamu (BHRT) limewataka wananchi mkoani Manyara kuwatumia Wasaidizi wa Kisheria kuwasaidia kifahamu haki zao za umiliki wa ardhi
Na George Augustino
Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kuwatumia wasaidizi wa kisheria kutoka Mashirika kama CSP pamoja na haki madini yanayofanya kazi mkoani Manyara wanaoshirikiana na Shirika la Bishara na Haki za Binadamu (BHRT) ili kuwasaidia kutatua changamoto zao za ardhi pamoja na kufahamu haki zao za umiliki wa Ardhi.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Shirika la Biashara na Haki za Binadamu (BHRT) Rose Ugulumu alipozungumza na fm Manyara, amesema (BHRT) inafanya kazi pamoja na mashirika yaliyopo mkoani Manyara Serikali pamoja na wadau wengine katika kuwasaidia wananchi kuwa na uelewa wa kisheria na kutambua haki zao katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Ardhi.
Kwa upande wake Erick Luwongo kutoka taasisia ya Haki Madini pamoja na Eleakimu Paulo kutoka Shirika la CSP mkoani Manyara wamesema kila mwananchi ana haki ya kumiliki ardhi kwa mujibu wa sheria kwa kufuata utaratibu unao hitajika kisheria.
Akizungumza kuhusu fidia ya eneo la Mwananchi lililotwaliwa na Serikali au Muwekezaji Afisa miradi kutoka (BHRT) Hussein Mvovo amesema mwananchi anaweza akapewa ardhi mbadala yenye ubora sawa na iliyotwaliwa, fedha au jengo linalofanana ukubwa na ubora na fidia hizo zinatakiwa zilipwe ndani ya miezi sita.
