FM Manyara
FM Manyara
2 October 2026, 5:15 pm

Klinik ya Ushirika iliyokuwa ikiendelea mkoani Manyara imetamatika leo ambapo wananchi wamenufaika kwa kupata fursa ya kuwasilisha na kutatuliwa changamoto mbalimbali zinazohusiana na masuala ya ushirika.
Na Mzidalfa Zaid
Kufuatia kuwepo kwa klinik ya ushirika mkani Manyara kwa siku tatu, wananchi mkoani Manyara wamenufaika na klinic hiyo bada ya kutatuliwa changamoto mbalimbali.
Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Manyara, Absalom Cheliga, amesema katika siku zote za klinik hiyo wamepokea wananchi wengi waliowasilisha kero mbalimbali ambazo zimetatuliwa pamoja na utoaji wa elimu ya ushirika .
Kwa upande wake Wakili wa Serikali Mfawidhi Mkoa wa Manyara Lameck Butuntu amesema ameshiriki katika kliniki hiyo kama mdau wa haki ambapo walipokea, kutoa ushauri na kushughulikia kesi mbalimbali zilizowasilishwa na wananchi.

Nao baadhi ya wananchi walionufaika na kliniki hiyo wamesema imewasaidia kupata ufumbuzi wa changamoto mbalimbali walizokuwa wakikabiliana nazo, huku wakishukuru Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kuleta kliniki hiyo mkoani Manyara.
Kampeni hiyo ya “Linda Ushirika, Chagua Uadilifu” imelenga kuongeza uelewa wa wadau kuhusu Sheria ya Ushirika, kanuni, miongozo na taratibu za usimamizi wa vyama vya ushirika, pamoja na kuimarisha uadilifu, uwajibikaji na utatuzi wa migogoro katika sekta ya ushirika.