FM Manyara

BHRT suluhu ya migogoro ya Ardhi Manyara

25 September 2026, 5:52 pm

Picha ya Mkurugenzi wa Shirika la Biashara na haki za Binaadamu  BHRT Rose Ugulumu (Picha na Hawa Rashidi)

 Shirika  la Biashara na Haki za Binaadamu  BHRT limeendelea kutoa elimu mbali mbali kuhusu haki za binaadam  katika uwekezaji wa biashara na  haki ya  ardhi

Na Hawa Rashidi

Mkurugenzi wa Shirika la Biashara na haki za Binaadamu  BHRT Rose Ugulumu Ameiomba Serikali   kutoa elimu ya huduma za kisheria kwa viongozi wa dini, vijana, wasaidizi wa kisheria mashiririka  mbali mbali  pamoja na viongozi wa kimila  kusaidia  kulinda haki za binaadamu  na kuziheshimu. 

Mkurugenzi  wa shirika hilo  Rose Ugulumu ameyasema hayo September 24 2026 wakati akihitimisha mafunzo ya siku mbili yakuwajengea uwezo wananchi, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali viongozi wa ngazi ya kijiji na viongozi wa kimila katika suala zima la haki ya ardhi yaliyoandaliwa na shirika hilo katika ukumbi wa White Rose uliopo mjini Babati  mkoani Manyara,ambapo  amesema kumekuwa na uwelewa mdogo kwa jamii kuhusu suala la kumiliki ardhi.

sauti ya Mkurugenzi wa Shirika la Biashara na haki za Binaadamu  BHRT Rose Ugulumu

Kwa upande wake Afisa Miradi  wa Shirika hilo  Husein Vomvo amesema  Shirika hilo limeendelea kutoa elimu mbali mbali kuhusu haki za binaadam katika uwekezaji wa biashara,  na kupitia mafunzo hayo yameleta mafanikio makubwa miongoni mwa washiriki  wengi  ambao walikuwa  na uelewa kuhusu haki ya  ardhi lakini  kwa kiasi kikubwa hawafahamu  masuala ya uthamini, fidia na utatuzi wa malalamiko hususani katika  masuala ya ardhi  ambapo washiriki hao wameomba  elimu  hiyo ifike katika maeneo mengine ya mkoa  wa Manyara ikiwemo wilaya  za kiteto  na Simanjiro.

Sauti ya Afisa Miradi  wa Shirika la BHRT

Aidha  Ameiomba  serikali kuweka utaratibu mzuri wa  kutoa fidia mapema  kwa wananchi ambao wanapitiwa na miradi ya serikali kutokana na wananchi wengi kutokujua sheria za Ardhi na kuangalia namna bora juu ya utatuzi wa migogoro hiyo kwa wanachi ili kuondoa minong^ono baina ya wananchi na Seikali.

Kwa upande wao wasaidizi wa kishria walioshiriki mafunzo hayo kutoka mkoa wa Manyara na Arusha wamelipongeza shirika la BHRT  kwa kutoa mafunzo hayo na kuliomba kupanua wigo mpana wa kuendeleakutoa elimu katika maeneo mbali mbali  ya mkoa wa Manyara na kuwajengea uwezo  katika kutekeleza majukumu yao ya kuwahidumia wanachi , na kuahidi kuyatumia  mafunzo hayo  kutoa elimu kwa wanachi  ambapo  wananchi wengi hawazifahamu sheria  za umiliki ardhi.

Sauti za wasaidizi wa kishria

Picha ya washiriki wa warsha ya haki ya ardhi