FM Manyara

Uhamiaji Manyara wataka ushirikiano kudhibiti wahamiaji wasiofuata sheria

28 September 2026, 7:15 pm

Picha ya Mkaguzi wa Uhamiaji mkoa wa Manyara Awadhi Killo

Wananchi mkoani Manyara wametakiwa kushirikiana na Serikali katika kudhibiti uwepo wa wahamiaji wasiofuata taratibu za kisheria nchini kuelekea AFCON.

Na Emmy Peter

Idara ya Uhamiaji mkoani Manyara imetoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa wananchi kushirikiana na Serikali katika kudhibiti uwepo wa wahamiaji wasiofuata taratibu za kisheria nchini, hususani katika kipindi ambacho Tanzania inajiandaa kwa shughuli mbalimbali zinazohusiana na mashindano ya AFCON.

Mkaguzi wa Uhamiaji mkoa wa Manyara Awadhi Killo amesema hatua hiyo inalenga kuimarisha usalama, kulinda amani na kuhakikisha shughuli mbalimbali za kijamii, kiuchumi na michezo, ikiwemo maandalizi kuelekea AFCON, zinafanyika katika mazingira salama.

Sauti ya Mkaguzi wa Uhamiaji mkoa wa Manyara Awadhi Killo

Aidha, Killo amewahimiza wananchi kuendelea kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kuhakikisha wageni wanaoingia na kuishi nchini wanafuata sheria na taratibu zilizowekwa.

Sauti ya Mkaguzi wa Uhamiaji mkoa wa Manyara Awadhi Killo

Idara ya Uhamiaji imeendelea kusisitiza kuwa jukumu la kulinda usalama wa nchi ni la pamoja, hivyo wananchi wanapaswa kuwa sehemu ya kutoa taarifa sahihi kwa mamlaka pale wanapobaini viashiria vya ukiukwaji wa sheria na taratibu za uhamiaji.