FM Manyara

Wananchi Manyara watakiwa kuzingatia kanuni za afya

26 October 2026, 10:20 pm

Picha ya afisa afya mkoa wa Manyara

Wananchi Manyara  watakiwa kuzingatia usafi wa mikono kwa kutumia maji tiririka na sabuni, pamoja na kutoa taarifa kwa mamlaka za afya wanapobaini dalili zinazoweza kuashiria ugonjwa wa Ebola

Emmy Peter

Wananchi wa mkoa wa Manyara wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Ebola ulioripotiwa  katika nchi jirani, kwa kuzingatia kanuni  za afya  ikiwemo kuepuka kushikana mikono na kukumbatiana ili kupunguza  hatari ya maambukizi.

Akizungumza na Fm Manyara  kuhusu tahadhari hizo, Afisa afya wa mkoa wa manyara, Switen Mwabulambo, amesema ni muhimu kwa wananchi kuendelea kuwa makini na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya ili kujikinga na ugonjwa huo.

Aidha, amewataka wananchi  kuendelea kuchukua tahadhari  na kupata taarifa  sahihi kutoka kwa wataalamu wa afya badala ya kutegemea taarifa zisizothibitishwa

Sauti ya afisa afya mkoa wa Manyara