FM Manyara

Wazazi Manyara watakiwa kuwalinda watoto dhidi ya ukatili kipindi cha likizo

12 November 2026, 8:03 pm

Picha ya afisa ustawi wa jamii mkoa wa Manyara Hadija Muwango

Wazazi na walezi Mkoani Manyara wametakiwa kuongeza uangalizi kwa watoto wao katika kipindi hiki cha likizo ili kuwalinda dhidi ya vitendo vya ukatili vinavyoweza kujitokeza katika maeneo mbalimbali.

Na Mzidalfa Zaid

Katika kipindi hiki ambacho wanafunzi wanaanza likizo, wazazi na walezi mkoani Manyara wametakiwa kuwa karibu na watoto wao na kwa kuwalinda dhidi ya ukatili ambao wanaweza kufanyiwa na watu wao wa karibu.

Wito huo umetolewa leo na Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Manyara, Hadija Muwango, wakati akizungumza na FM Manyara amesema kipindi cha likizo ni wakati ambao watoto hutumia muda mwingi wakiwa nyumbani au katika maeneo mbalimbali nje ya shule, hali inayohitaji wazazi na walezi kuwa karibu nao na kufuatilia mienendo pamoja na mazingira wanayokutana nayo.

Sauti ya Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Manyara, Hadija Muwango

Aidha, amewataka wazazi kutowapa watoto uhuru usio na mipaka na badala yake kuhakikisha wanakuwa katika mazingira salama wakati wote wa likizo.