FM Manyara
FM Manyara
20 July 2026, 4:49 pm

Watanzania wametakiwa kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano,kwakua ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa pamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali katika sekta ya elimu.
Na Emmy Peter
Mbunge wa Babati mjini ambae ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Daniel Barani Sillo amewataka watanzania kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano, akisisitiza kuwa mazingira ya amani ndiyo msingi wa maendeleo ya taifa pamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali katika sekta ya elimu.
Silo ametoa kauli hiyo wakati akichangia harambee ya ujenzi wa shule ya msingi ya kiislamu inayojengwa katika Halmashauri ya wilaya ya Babati mkoani Manyara, amesema wadau wa maendeleo wanapaswa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali, hususan katika sekta ya elimu, ili kuhakikisha watoto wanapata mazingira bora ya kujifunzia na elimu bora

kwa upande wake, Sheikh wa mkoa wa Manyara Mohamed Kadidi amesema waumini wanapaswa kuendelea kuilinda amani ya nchi na kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule hiyo ambayo itachangia kutoa elimu bora pamoja na malezi yenye maadili mema kwa watoto.
Aidha baadhi ya wananchi waliohudhuria harambee hiyo wameishukuru Bakwata kwa kuanzisha wazo la ujenzi wa shule hiyo, wakisema litakuwa na manufaa makubwa kwa jamii na itasaidia kuandaa kizazi chenye elimu, maadili na uzalendo.